Main Article Content
UTANDAWAZI NA DHIMA YA KISWAHILI KAMA LUGHA YA AFRIKA MASHARIKI
Abstract
Neno “utandawazi” limevuma na kusambaa kwa kasi kubwa kati ya maneno mapya yaliyoibuka enzi za karibuni katika lugha ya Kiswahili. Kusambaa kwa neno hili ni ushahidi tosha kwamba dhana ya utandawazi inayobebwa na neno hili inagusa nyanja mbalimbali za maisha katika jamii – siasa, uchumi, uandishi wa habari, elimu, utamaduni, sayansi na tekinolojia na nyanja nyingi nyinginezo. Kutokana na kusambaa huko katika matumizi inawezekana neno “utandawazi” likawa na maana zinazotofautiana kidogo kutoka uwanja hadi uwanja. Katika kutazama fasili mbalimbali za neno hilo, makala hii inabainisha kuwa tunaweza kujua ipi ni dhana ya msingi ambayo huzingatiwa hata kama pengine maelezo ya maana ya neno hutofautiana kutoka uwanja hadi uwanja. Makala inaonyesha kuwa nyingi kati ya fasili zilizowahi kutolewa huyagusa maisha ya wanajamii wengi katika jamii mbalimbali hasa katika nyaja za uchumi, siasa na utamaduni kwa jumla ambamo lugha hupata nafasi ya pekee.