Main Article Content

Ujanibishaji wa Office 2003 na Windows XP kwa Kiswahili Sanifu


Kulikoyela Kahigi

Abstract

Mradi wa ujanibishaji wa Office 2003 na Windows XP kwa Kiswahili sanifu ulitekelezwa katika kipindi 2004-2005. Malengo ya mradi yalikuwa: (1) kuandaa istilahi za kompyuta kwa Kiingereza-Kiswahili, na (2) kutafsiri programu nne za kawaida za Office (Outlook, Excel, Word na PowerPoint) na Windows XP.

Makala hii ina madhumuni yafuatayo: kwanza, kutoa taarifa kuhusu shughuli ya ujanibishaji wa Office 2003 na Windows XP; pili, kueleza misingi ya uundaji wa istilahi ambayo waundaji istilahi walikubali kuitumia, na istilahi zilizoundwa kwa kuitumia; tatu, kuchunguza changamoto za tafsiri kwa kutumia zana zilizokuwa zimeandaliwa (istilahi, mwongozo wa mtindo, na mwongozo wa kitamaduni au stara), na mwisho kueleza baadhi ya changamoto na matatizo ambayo waundaji istilahi na wafasiri walikumbana nayo katika utekelezaji wa mradi huo. Makala inahitimisha kwa kutoa mapendekezo kuhusu mambo ambayo yanapaswa kuzingatiwa katika ujanibishaji wa baadaye.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X