Main Article Content
Muundo na matumizi ya umiliki siachanifu kwa Kiswahili sanifu
Abstract
Katika Kiswahili sanifu inawezekana kuzungumza kuhusu kiumbe hai, mwili wake na hisia zake kwa njia mbalimbali. Njia iliyotumiwa kuliko zote ni umiliki siachanifu kwa sababu mwili na sehemu zake ni kitu kimoja. Pia, upande wa kiisimu, umiliki siachanifu una mambo yake ya pekee ya kisarufi miundo. Makala hii, kwanza inazingatia sababu za kutumiwa kwa umiliki siachanifu; pili inazingatia mabadiliko yaletwayo na umiliki siachanifu kwenye valensi ya vitenzi. Makala haichambui kabisa masuala ya kirai nomino. Inauliza tu kwa nini msemaji Mswahili hupendelea namna hii ya kusema wakati ambapo angeweza kutumia kanuni za kawaida za sarufi-miundo kuzungumzia mambo hayo hayo.