Main Article Content

Uhalisiamazingaombwe katika fasihi ya Kiswahili: Istilahi mpya, mtindo mkongwe


F.E.M.K Senkoro

Abstract

Makala hii inaichambua dhana ya Uhalisiamazingaombwe kama ambavyo imekuja kutumika hivi karibuni miongoni mwa wandishi na wahakiki wa fasihi ya Kiswahili. Pamoja na kutoa mifano ya kazi mbalimbali za fasihi ya Kiswahili ambamo mna mtindo wa Uhalisiamazingaombwe, uchambuzi katika makala hii unatumia zaidi hadithi fupi ya Said Ahmed Mohamed ya “Sadiki Ukipenda” na riwaya fupi ya E. Kezilahabi ya Nagona kama vielelezo vya namna Uhalisiamazingaombwe ulivyotumika katika kazi za fasihi ya Kiswahili. Swali ambalo makala hii inaliibua na kujaribu kulijibu ni je, ni kweli kuwa, kama anavyodai Said Ahmed Mohamed, Uhalisiamazingaombwe ni mtindo wa hivi karibuni tu na kwamba ndiyo kwanza dhana hii imeanza kushika kasi miongoni mwa waandishi wa fasihi ya Kiswahili, au ni istilahi mpya tu inayoelezea mtindo mkongwe?

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X