Main Article Content
VIDOKEZO VYA MOFOLOJIA YA KITENZI KATIKA LUZINZA
Abstract
Lengo la makala hii ni kutoa maelezo mafupi ya sarufi ya lugha ya Luzinza ikizingatiakipengele cha mofolojia ya kitenzi. Huu utakuwa mwanzo wa kuchochea uandishi wa kina wa sarufi ya lugha hii. Mfuatano wa viambishi (mofimu) mbalimbali vinavyounda kitenzi umeelezwa ukijumuisha mofimu tangulizi, mzizi, na mofimu fuatishi, yaani mofimu nyambulishi za kitenzi. Aidha kipengele cha kutengamana kwa mofimu kimeelezwa kwa kuzingatia minyambuliko ya vitenzi vya silabi moja na silabi zaidi ya moja. Pametolewa pia maelezo mafupi na mifano ya dhana ya uradidi wa mizizi; na vielelezo vya mofimu zinazonyambuliwa kutokana na nomino na maneno mengineyo. Makala hii inahitimishwa na maelezo mafupi ya vipengele ambavyo havikuguswa (kutokana na ufinyu wa makala yenyewe) ili vielezwe kwa kinagaubaga na watafiti wengineo.