Main Article Content
Kiswahili nchini Kenya: ukuaji au ukiushi?
Abstract
Makala hii inadondoa baadhi ya mifano ya miundo ya maneno pamoja na uvunjaji wa mfuatano wa kisarufi unaobainika katika baadhi ya wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili nchini Kenya. Makala inahoji kama haya ni maendeleo ya lugha au ni njia mojawapo ya kuidumaza isiweze kuchukua nafasi yake kama lugha ya taifa nchini. Katika sehemu ya mwisho ya makala, yanatolewa mapendekezo ambayo yamekusudiwa kusahihisha hali iliyopo ili kukifanya Kiswahili kama lugha muhimu nchini Kenya, iweze kujitanua kimatumizi na kurejesha hadhi yake kama lugha ya walio wengi nchini humo.