Main Article Content
LUGHA KAMA KITAMBULISHO: CHANGAMOTO YA “SHENG” NCHINI KENYA
Abstract
Makala hii inajadili suala la lugha na utambulishaji wa utamaduni. Inasisitizwa katika makala hii kwamba iwapo lugha itachukuliwa kuwa ni kielelezo na nyenzo ya utamaduni wa kitaifa, basi, katika muktadha wa Kenya ya sasa, kielezo hicho kinatetereka kutokana na hali ya kutatanisha ya lugha nchini humo. Utata huu unadhihirishwa na kuzuka kwa msimbo wa vijana uitwao’ “Sheng” ndiko chanzo cha utata huo wa kilugha na kitamaduni, na makala inasisitiza kuwa hali hii ni ishara ya vijana kutokuridhika kitamaduni katika jamii ya kisasa. Makala inamalizia kwa kueleza haja iliyopo ya kuunda upya sera ya kitaifa ya lugha itakayofafanua hadhi na majukumu ya lugha za kigeni kama Kiingereza kwa upande mmoja na Kiswahili na lugha zingine za kiasili kwa upande mwengine.