Main Article Content
MTINDO KATIKA RIWAYA YA SIKU YA WATENZI WOTE
Abstract
Makala hii inachambua mtindo katika riwaya ya Siku ya Watenzi Wote kwanza kwa kutoa ufafanuzi wa mitazamo mbalimbali juu ya dhana ya mtindo. Makala inatumia mitazamo jumuishi ya mtindo kama uteuzi na mtindo kama tofauti. Katika kufanya uchambuzi wa mtindo wa riwaya hii, mhakiki amezama katika vipengele vya matumizi ya uwili, matumizi ya ushairi na matumizi ya vilugha. Vipengele hivi ndivyo ambavyo vinatumiwa na Shaaban Robert kudhihirishia maudhui ya kazi yake ; na umuhimu wa maudhui hayo kwa jamii ya leo unadhihirika hata kama Shaaban Robert aliandika kazi yake zaidi ya miaka hamsini iliyopita.