Main Article Content

Ujitokezaji na Dhima za Yambwa katika Muundo wa Utendea wa Kimatengo na Kiswahili


Fokas Nchimbi

Abstract

Miundo mbalimbali ya vitenzi vya lugha za Kibantu huweza kuamua ruwaza za utokeaji na dhima za kisemantiki za nomino za yambwa. Makala hii inachunguza mazingira ya utokeaji wa nomino za yambwa na dhima zake za kisemantiki katika lugha za Kimatengo na  Kiswahili katika muundo wa kati wa utendea. Kufikia malengo hayo, makala hii inaongozwa na Nadharia ya Sarufi ya Uamilifu wa  Kileksika inayomakinikia miundo miwili ya kisintaksia, yaani muundo wa kisintaksia unaowasilisha mfuatano wa maneno na makundi ya  virai. Pili, muundo wa kisintaksia unaowasilisha uamilifu wa kisintaksia, kama vile kiima na yambwa. Data za utafiti huu zilikusanywa kwa  njia kuu mbili. Data zinazohusu lugha ya Kimatengo zilipatikana uwandani kwa kuwatumia wazungumzaji asilia wa lugha hiyo. Data za  Kiswahili zilikusanywa kutoka katika matini mbalimbali. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwapo kwa aina mbili za yambwa katika  muundo wa utendea katika Kimatengo na Kiswahili, yaani yambwa tendewa na yambwa tendwa. Yambwa hizo zinazojitokeza baada ya  kitenzi tendea zina dhima mbalimbali za kisemantiki ambazo ni unufaika, uathirika, uelekeo, kifaa na sababu. 


Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X