Main Article Content

Mwelekeo wa Usarufishaji wa Nomino za Kiswahili zenye Asili ya Kiingereza na Kiarabu


Johari Hakimu

Abstract

Makala hii inaonesha mwelekeo wa usarufishaji wa nomino za Kiswahili zenye asili ya Kiingereza na Kiarabu. Mwelekeo wa nomimo hizo  umeoneshwa kwa kutumia data iliyokusanywa kwa njia ya upitiaji wa nyaraka. Nyaraka zilizopitiwa ni Kamusi Kuu ya Kiswahili (2022) na  Kamusi ya Karne ya 21 (2021). Data iliyopatikana ilichanganuliwa kwa kutumia Nadharia ya Mofolojia ya Ongezeko la Maneno na kufafanuliwa kwa kutumia Nadharia ya Usarufishaji. Uchanganuzi na ufafanuzi wa data hizo umeonesha kuwa kuna mielekeo chanya na  hasi ya usarufishaji wa nomino za Kiswahili kwa kuzingatia ngeli za majina. Mwelekeo chanya wa usarufishaji wa nomino za Kiswahili zenye asili ya Kiingereza na Kiarabu umeonesha mchakato wa usarufishaji uliokamilika katika Kiswahili. Mwelekeo hasi umedhihirisha  usarufishaji usiokamilika katika baadhi ya nomino za Kiswahili zenye asili ya Kiingereza na Kiarabu. Kwa ujumla, ufafanuzi wa nomino za  Kiswahili unapaswa kuzingatia mazingira ya namna zinavyojitokeza na kusarufishwa katika lugha hii.  


Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X