Main Article Content

Uchanganyaji Msimbo katika Jamiilugha za Mitandaopepe:Mtagusano wa Kiswahili na Kiingereza


Rhoda P. Kidami

Abstract

Mitandaopepe2 imetoa fursa kwa watu kutagusana katika masuala anuwai ya kijamii. Kiswahili ni miongoni mwa lugha zinazotumiwa katika mitandaopepe, ndani na nje ya Tanzania. Kutokana na kukua na kusambaa kwa lugha hiyo ulimwenguni kote, kuna haja ya  kuchunguza mwonekano wake katika muktadha huo wa kimawasilianopepe. Lengo la makala hii ni kuchunguza jinsi Kiswahili  kinavyotagusana na lugha ya Kiingereza katika mawasiliano hayo, hususani kwenye kipengele cha uchanganyaji msimbo. Data za utafiti  huu ni maoni yaliyotolewa kwenye mtandao wa YouTube baada ya watu kusikiliza hotuba za Kiswahili za Mwalimu Nyerere. Jumla ya  maoni elfu mbili na sitini yalikusanywa kutoka katika hotuba tatu. Uchanganuzi wa data hizo uliongozwa na Kiolezo cha Myers-Scotton  (2001) kinachohusu lugha msingi na lugha changiaji katika kipengele cha uchanganyaji msimbo. Matokeo ya utafiti yamedhihirisha  kwamba lugha za Kiswahili na Kiingereza zinakamilishana katika muktadha wa kimawasilianopepe. Katika miktadha tofautitofauti, lugha  mojawapo imetumiwa kuwa msingi wa mawasiliano huku nyingine ikijaliza sarufi ya lugha msingi. Wakati mwingine, lugha zote mbili  zimetumiwa kwa pamoja huku kila moja ikijikamilisha kisarufi. 


Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X