Main Article Content

Tofauti za Kifonolojia na Kimsamiati baina ya Kiswahili cha Kigoma, Ujiji na Kiswahili Sanifu


Ahmad Y. Sovu

Abstract

Watanzania wengi, hususani waishio vijijini, wana lugha zao za asili ambapo hujifunza Kiswahili na kukitumia kama lugha ya pili. Watanzania hao, wanapotumia Kiswahili huonekana wakibadili baadhi ya sauti na maneno. Makala hii inalenga kuchunguza tofauti za kifonolojia na kimsamiati baina ya Kiswahili cha Kigoma Ujiji na Kiswahili sanifu ili kubaini tofauti za matumizi ya sauti na maneno kati ya  lugha hizo. Data zimekusanywa kwa kutumia ushuhudiaji na majadiliano ya vikundi. Uchambuzi na uwasilishaji wa data umeongozwa na  Mkabala wa Mbinu Linganishi (Anttila, 1972). Matokeo ya uchunguzi yanaonesha kuwa kuna tofauti ya kifonolojia baina Kiswahili cha  Kigoma, Ujiji na Kiswahili sanifu katika sauti zenye maneno yenye asili ya kigeni kama vile sauti [h], [bu], [mu]. Pia, kuna tofauti ya  mabadiliko ya sauti [a] badala ya sauti [ha], [s] kuwa [sh], [r] badala ya [l], [bh] badala ya [b] na [bu] au [tu] kuwa [wa]. Aidha, kuna tofauti  za matumizi ya sauti [-ga], lafudhi na mabadiliko ya kialami [ngo] badala ya sauti [eti] na tofauti za urefushaji irabu. Katika  muktadha huo, Kiswahili cha Kigoma, Ujiji kinafanana na kutofautiana na Kiswahili sanifu kifonolojia na kimsamiati. Hata hivyo, tofauti  zilizobainika ni zile za ubadilishaji wa sauti na msamiati usio wa msingi katika lugha hizo ambazo kwa kiasi kikubwa zinatokana na athari  za lugha mama.  


Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X