Main Article Content

Mabadiliko ya Utambulisho wa Mwanamke na Uimarishaji wa Ujinsuke: Mifano kutoka Riwaya ya Nyuso za Mwanamke (Mohamed, 2010)


Ernesta S. Mosha

Abstract

Tafiti mbalimbali kuhusu riwaya ya Kiswahili zinaonesha kuwa mwanamke amesawiriwa kwa mitazamo mbalimbali, ukiwamo mtazamo  hasi. Usawiri wa mtazamo huo unamtambulisha mwanamke kama kiumbe dhaifu na duni. Kwa kuongozwa na Nadharia ya Udenguzi,  makala imeonesha namna mhusika mwanamke anavyoweza kubadilisha utambulisho hasi na kujenga utambulisho chanya. Makala imetumia data kutoka katika riwaya ya Nyuso za Mwanamke (Mohamed, 2010) zilizopatikana kwa usomaji makini. Makala imeweka  bayana nafasi ya riwaya ya Kiswahili katika kujenga utambulisho wa mwanamke unaoimarisha ujinsuke2 . Matokeo haya yanatokana na  uumbaji wa wahusika wanawake wanaodengua kaida za jamii zinazomkandamiza mwanamke na kufichua mbinu zinazotumiwa na  baadhi ya wanajamii kuendeleza ukandamizaji huo. Pia, umuhimu wa wanawake kujitambua na kujisimamia umewekwa bayana.  


Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X