Main Article Content

Miangwi ya Kimtindo, Kidhamira na Uhusika: Uchunguzi wa Kazi Teule


Kyallo W. Wamitila

Abstract

Makala hii inachunguza namna ambavyo kazi za kifasihi zinaakisi uhusiano na ufanano wa kimatini hasa katika kiwango cha mtindo, dhamira na usawiri na uendelezaji wa wahusika. Msingi wake mkuu ni imani kuwa fasihi inahusiana na fasihi na matini na kazi  mbalimbali huingiliana, kuathiriana, kutagusana na kujalizana katika mwanda wa kimwingilianomatini. Matini za kimsingi ambazo  zimechunguzwa ni tamthiliya mbili (Mashetani ya E. Hussein na Mashetani Wamerudi ya S.A. Mohamed), hadithi fupi ya “Mke Wangu” ya  M.S. Abdulla na riwaya ya Wenye Meno ya S.A. Mohamed, zilizoteuliwa kimakusudi. Uchunguzi huo umefanywa kwa kuzingatia mawazo  ya Nadharia ya Mwingilianomatini inayohusishwa na Julia Kristeva aliyebuni dhana hii mwaka 1966. Kristeva aliyakuza mawazo yake  kwenye msingi wa dhana ya usemezano inayohusishwa na mwanaisimu, mwanafasihi na mwanafalsafa wa Kirusi, Mikhail Mikhailovich  Bakhtin. Makala hii imebainisha sifa na viwango mbalimbali vya udhihirikaji huo wa mwingiliano na kuzungumzia athari zake katika  uendelezaji wa maana ya kifasihi na fasiri za kifasihi zinazofuatia. 


Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X