Main Article Content
Mkengeuko wa Malezi kwa Wahusika katika Riwaya ya Rosa Mistika
Abstract
Makala hii imechunguza mkengeuko wa malezi wa wahusika katika riwaya ya Rosa Mistika. Data za makala zimepatikana maktabani kwa mbinu ya usomaji makini wa matini ya riwaya husika na kisha kuchambua data hizo kwa mkabala wa kimaudhui na kuziwasilisha kwa mkabala wa kitaamuli. Makala imeongozwa na misingi ya Nadharia ya Sosholojia ya Kifasihi katika ukusanyaji na uchambuzi wa data. Matokeo yanaonesha kuwapo kwa matukio mengi ya wahusika kukengeuka malezi katika riwaya hii. Matukio hayo ni ubakaji, kujiua, rushwa, umalaya, kupuuza ushauri na matusi. Matukio haya yameoneshwa katika kazi husika kwa kuwa ni mwakiso wa uhalisi wa kijamii kama Nadharia ya Sosholojia ya Kifasihi inavyofungamanisha jamii na kazi za fasihi.