Main Article Content

Mtindo wa Usambamba katika Utenzi wa Seyidina Ali na Mudhari bin Darimi


Adria Fuluge

Abstract

Katika makala hii tumechunguza aina mbalimbali za usambamba na mchango wake katika Utenzi wa Seyidina Ali na Mudhari bin Darimi. Ili kufanikisha hili, makala imeongozwa na Nadharia ya Umitindo ambayo inachunguza na kutoa fasiri kwa kazi za isimu na fasihi. Nadharia hii imetumika katika makala hii kwa kuwa uchunguzi wa vipengele vya kifasihi hutegemea vile vya kiisimu. Nadharia ya Umitindo inahusishwa na Geoffrey Leech (1969) hasa katika andiko lake la A Linguistic Guide to English Poetry. Lengo la uhakiki wetu ni kuweka wazi aina mbalimbali za usambamba zinazobainika katika utenzi huu na michango yake katika kufanikisha fani na maudhui kwenye utungo huu. Kutokana na uchunguzi wetu, tumebainisha kuwa matumizi ya usambamba kama aina ya urudiaji yanachangia  katika ukuzaji na uendelezaji wa dhamira, usawiri na ujenzi wa wahusika na kuingiliana na sifa nyingine za kimtindo ili kuibua umbuji wa  kijumla wa utungo huu. 


Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X
 
empty cookie