Main Article Content

Matumizi ya Fantasia katika Fasihi ya Kiswahili Yanavyoibua, Kujenga na Kuwasilisha Dhamira


Gerephace Mwangosi

Abstract

Makala hii imechunguza namna kipengele cha fantasia katika fasihi ya Kiswahili kinavyoibua, kujenga na kuwasilisha dhamira. Lengo la makala hii ni kuchunguza namna kipengele cha fantasia kinavyotumika kuibua, kujenga na kuwasilisha dhamira katika riwaya ya  Kiswahili. Data za msingi zilipatikana katika riwaya teule ya Kusadikika kwa mbinu ya usomaji makini. Nyaraka zilizotumika kufafanua na kuthibitisha data za msingi zilipatikana kwa mbinu ya kielektroniki na kimaktaba. Uchambuzi na mjadala wa data uliongozwa na Nadharia  ya Semiotiki. Msingi mkuu wa nadharia hii ni kushughulika na ishara pamoja na uashiriaji katika kazi za fasihi. Matokeo ya  utafiti yamewasilishwa kwa mbinu ya kimaelezo. Matokeo yameonesha namna msuko wa fantasia katika kitabu teule unaivyoibua  dhamira zinazolenga kuifunza, kuiimarisha na kuiweka jamii pamoja katika misingi imara ya utamaduni, siasa na uchumi. Dhamira  zilizoibuliwa zinawasilisha matendo ya msingi ya binadamu yanayojidhihirisha katika nyanja zote za maisha na maendeleo yake. Kwa  hiyo, makala hii inapendekeza kuwa utafiti ufanyike zaidi katika tanzu za fasihi simulizi ya Kiswahili kuhusu matumizi ya fantasia  yanavyofumbata masuala ya uchumi, siasa, utamaduni, falsafa na itikadi za jamii. 


Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X
 
empty cookie