Main Article Content

Uchambuzi wa Mashartizuizi katika Muundo wa Silabi za Kichasu


Rabiel Fadhili
Faraja Mwendamseke

Abstract

Makala hii imechunguza muundo wa silabi za lugha ya Kichasu kwa kuzingatia uchambuzi wa mashartizuizi ya Kichasu. Lengo la makala hii ni kubainisha miundo ya silabi za lugha hiyo. Utofauti wa udhihirikaji wa miundo ya silabi katika lugha mbalimbali za Kibantu ndio  umechagiza kufanyika kwa utafiti huu. Kutokana na tafiti mbalimbali, kila lugha huwa na mpangilio tofauti wa mashartizuizi na ujitokezaji  wa miundo yake huweka mipaka katika miundo ya silabi zake katika maneno. Data zilikusanywa kwa kutumia upitiaji  maandiko pamoja na masimulizi kutoka kwa watoataarifa. Data zilichanganuliwa kwa mkabala wa kitaamuli ambapo mbinu ya  uchanganuzi kimada imetumika. Uchanganuzi wa data uliongozwa na misingi ya Nadharia ya Umbo Upeo (1993). Matokeo yanaonesha  kwamba Kichasu kina jumla ya miundo kumi na mmoja ya silabi inayokubalika kisarufi. Miundo hiyo ni ya silabi nyepesi na ya silabi nzito.


Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X
 
empty cookie