Main Article Content
Athari za Kinyarwanda katika Ufundishaji na Ujifunzaji wa Kiswahili katika Shule Teule za Sekondari Wilayani Gakenke, Rwanda
Abstract
Makala hii inachunguza jinsi Kinyawanda kinavyoathiri ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili. Watoataarifa 24 ambao ni wanafunzi 18, walimu 3 pamoja na wakuu wa masomo 3, walitumiwa kuwa vyanzo vya taarifa. Data hizo zilikusanywa kupitia mahojiano, ushuhudiaji pamoja na udurusu wa nyaraka. Nadharia ya Utabia iliyoasisiwa na Skinner mwaka 1950 ndiyo iliyoongoza utafiti huu. Matokeo yanaonesha kwamba wanafunzi wanachanganya Kinyarwanda na Kiswahili kwa kuwa lugha hizi zina mfanano wa karibu kimatamshi, kiotografia na kisemantiki. Hivyo basi, makala hii inapendekeza yafuatayo: mosi, kuwe na vitabu vya ziada na kiada shuleni. Pili, ufundishaji wa Kiswahili uwe wa lazima kuanzia shule za chekechea hadi vyuoni. Tatu, Kiswahili kifundishwe katika michepuo yote kama ilivyo kwa lugha ya Kiingereza. Mwisho, kuwe na mijadala na midahalo shuleni ili kuboresha kiwango cha lugha ya Kiswahili miongoni mwa wanafunzi.