Main Article Content
Usukuku wa Ukolonia katika Mjadala wa Lugha ya Kufundishia nchini Tanzania
Abstract
Makala hii inahusu usukuku wa ukolonia unaotawala fikra za wasomi katika mjadala wa lugha ya kufundishia nchini Tanzania. Lengo lake ni kueleza kwa nini mapendekezo ya kubadilisha lugha ya kufundishia kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili yanapata ukinzani miongoni mwa wasomi nchini Tanzania. Data zilitokana na maoni ya wasomi kupitia kundi la WhatsApp la UDASA-MUCE. Kiunzi cha Ubadaukoloni kinachohoji ukamilifu wa ukombozi uliopatikana katika nchi nyingi zilizowahi kutawaliwa kimetumika kuongoza utafiti huu. Matokeo yanaonesha kwamba kuna usukuku wa ukolonia miongoni mwa wanazuoni unaoathiri fikra zao kuhusu lugha ya kufundishia licha ya juhudi za kuwazindua. Kwa hiyo, ukombozi dhidi ya ukolonia wa maarifa hasa miongoni mwa wasomi ni muhimu na ni suala linalopaswa kushughulikiwa kwa hatua za dharura ili kunusuru ubora wa elimu nchini Tanzania. Pendekezo ni kwamba serikali itumie madokezo ya sera yanayotokana na tafiti za kisayansi kwa ajili ya kufanya maamuzi kuhusu lugha katika elimu.