Main Article Content
Matumizi ya Nahau katika Ujarabati wa Mikakati ya Kisintaksia ya Usimbaji wa Fokasi katika Sentensi za Kiswahili
Abstract
Usimbaji wa fokasi katika sentensi za lugha za Kibantu hufanyika kwa kutumia mikakati mbalimbali ya kimofolojia, kisintaksia au kifonolojia (van der Wal, 2009; Yonenda, 2011; Morimoto, 2014; Ndumiwe, 2023). Aidha, kuna mbinu tofautitofauti zinazotumika kung’amua ikiwa mikakati madhukura inasimba fokasi au la. Mojawapo ya mbinu hizo ni matumizi ya nahau. Van der Wal (2016, 2021) alichunguza mbinu hiyo katika ung’amuzi wa usimbaji wa fokasi katika lugha za Kimakua (P31), Kizulu (S42), Kimatengo (N13), Kirundi (JD62), Kichangana (S53), Kiganda (JE15), Kinyakyusa (M31), Kibukusu (JD31c) na Kitharaka (E54). Hata hivyo, hakuna utafiti uliofanyika katika lugha ya Kiswahili (G42) kuhusu matumizi ya nahau katika ujarabati wa mikakati ya usimbaji wa fokasi. Kwa hiyo, lengo la makala hii ni kuhakiki mikakati ya kisintakisa ya usimbaji wa fokasi kwa kutumia nahau za Kiswahili. Data zimekusanywa kwa kutumia mbinu za usaili na upitiaji wa nyaraka. Data hizo zimechambuliwa kitaamuli kwa kuongozwa na Nadharia ya Vibadala vya Kisemantiki (Rooth, 2016). Utafiti huu umebainisha kuwa nahau za Kiswahili zikiundiwa sentensi kwa kutumia mikakati ya ukasimishaji, upinduzi wa viambajengo na utenguaji kushoto, maana ya nahau inatoweka. Kwa hiyo, utowekaji wa maana ya nahau huthibitisha kuwa mikakati husika hutumika kusimba fokasi katika lugha ya Kiswahili.