Main Article Content

Tafsiri ya Lugha ya Ishara katika Wema Hawajazaliwa: Mtazamo wa Ulinganifu wa Kimawasiliano


Birigitha N. John

Abstract

Tafsiri ni taaluma kongwe ambayo imekuwa ikifanyika katika nyuga mbalimbali kama vile sheria, utabibu na lugha. Tafiti nyingi zimekitwa katika matatizo ya tafsiri kwa ujumla. Wataalamu wa tafsiri, hususani za kifasihi kama vile Mkinga (2005), Malangwa (2010) na Mekacha (2013), wametafiti kuhusu mbinu na matatizo ya kutafsiri matini za kifasihi. Data za makala hii zimetokana na mbinu ya uchambuzi wa matini na usaili. Wafasiri tofauti wametafsiri kazi za kifasihi kwa kuzingatia usanaa uliomo kwenye kazi husika. Makala hii inamulika tafsiri  ya lugha ya ishara katika Wema Hawajazaliwa kwa kuzingatia mtazamo wa ulinganifu wa kimawasiliano. Wema Hawajazaliwa ni riwaya iliyotafsiriwa na Abdilatif Abdallah kutoka katika riwaya ya The Beautyful Ones are not Yet Born ya Ayi Kwei Armah. Makala hii iliongozwa na Nadharia ya Ulinganifu wa Kimawasiliano iliyoasisiwa na Nida (1964). Pamoja na wataalamu wengi kutafiti kuhusu matatizo ya tafsiri, bado tafsiri ya kifasihi haijafanyiwa tafiti za kutosha hususani katika lugha ya Kiswahili. Makala hii imebaini kuwa, mfasiri  huzingatia lugha ya ishara katika tafsiri ya matukio mbalimbali ya kiishara. 


Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X
 
empty cookie