Main Article Content
Ubainishaji wa Mitindo katika Methali za Wamasaaba nchini Uganda
Abstract
Makala hii inafafanua mitindo katika methali za Wamasaaba nchini Uganda. Lengo kuu la makala ni kueleza jinsi methali za Wamasaaba zinavyotumia mitindo mahususi kuwasilisha ujumbe kwa jamii. Utafiti huu umefanyika uwandani. Utafiti umeongozwa na Nadharia ya Uelewaji Ujumbe kwa kutumia lugha ya moja kwa moja. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa mitindo katika methali za Wamasaaba inahusiana na: uteuzi wa maneno, idadi ya maneno katika methali, matumizi ya maneno ya kawaida, urejeleaji wa vitu vya kawaida, matumizi ya lugha kisanaa na matumizi ya maelezo katika methali badala ya maswali.