Main Article Content
Ukarabati wa Mfuatano wa Irabu kama Sababu ya Muunganiko wa Maneno katika Gᴉrᴉmi
Abstract
Mfuatano wa irabu katika lugha nyingi za Kibantu haupendelewi katika mazungumzo. Huepukwa kwa kutumia ukarabati wa namna mbalimbali. Kwa hiyo, makala hii inahusu ukarabati unaofanyika ili kuepukana na kutumia irabu zinazofuatana katika mpaka wa kisintaksia, yaani baina ya maneno yanayofuatana katika Gᴉrᴉmi (F32). Nadharia ya Fonolojia Zalishi Asilia imetumika kuchambua na kujadili data za makala hii. Mbinu za kukusanya data zilizotumika katika utafiti huu ni mbili: mbinu ya uhakiki wa kisarufi na ya usaili. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba, katika Gᴉrᴉmi, ukarabati wa mfuatano wa irabu baina ya neno na neno hufanywa kwa kutumia michakato mitatu ya kifonolojia ambayo ni mvutano wa irabu, udondoshaji wa irabu na uyeyushaji wa irabu. Ukarabati huo hufanyika kurahisisha matamshi na mazungumzo. Kufuatia matokeo haya, makala inapendekeza tafiti zaidi kufanyika ili kubaini jinsi mifanyiko ya kifonolojia inavyokarabati matamshi ya maneno yanayohusisha mfuatano wa irabu katika lugha zingine, hasa za Kibantu.