Main Article Content
Uainishaji wa Ngeli za Nomino za Kivunjo Kimofolojia
Abstract
Makala hii inashughulikia uainishaji wa ngeli za nomino katika lugha ya Kivunjo na kubainisha idadi yake kimofolojia. Ili kutimiza malengo haya, mbinu ya usampulishaji nasibu pangilifu imetumika katika kuwateua watoataarifa ambao ni wazungumzaji wa Kivunjo. Data zimekusanywa kwa kutumia hojaji, usaili na ushuhudiaji. Mkabala mseto, yaani wa kimaelezo na kiidadi umetumika katika kuwasilisha na kuchanganua data za utafiti huu. Aidha, utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya Mofolojia Asilia (NMA) iliyopendekezwa na Dressler (1985) na Wurzel (1987). Pamoja na nadharia hii, mkabala wa Viambishi Awali vya Nomino umetumika kubainisha viambishi ngeli vya nomino katika misingi ya umoja na wingi. Hivyo, kwa kutumia Mkabala wa Viambishi Awali vya Nomino matokeo ya utafiti huu yamebainisha kuwa lugha ya Kivunjo ina ngeli 18.