Main Article Content

Uolezi katika kujenga utambulisho wa wahusika katika Riwaya za Nagona na Mzingile za Euphrase Kezilahabi


Leonard Flavian Ilomo

Abstract

Uolezi ni mbinu muhimu ya kinaratolojia katika kueleza mtazamo au mwono. Hii ni mbinu inayotofautisha baina ya nani anaona na nani anasimulia. Kimsingi, mbinu hii hutumika katika kujenga uelewa na mtazamo juu ya masuala mbalimbali katika matini simulizi (Flavian, 2021). Dhima mojawapo ya mbinu hii inayojitokeza kwa uwazi ni kumfanya msomaji aone jambo fulani na kisha achukue mtazamo ambao utamwezesha kuyatazama mambo kwa mwelekeo fulani. Hata hivyo, kutokana na uchambuzi wa riwaya za Nagona (Kezilahabi, 1990; 2011) na Mzingile (Kezilahabi, 1991; 2011) ambao tumeufanya katika makala hii, uolezi unaonekana kutumika kujenga utambulisho wa wahusika. Katika makala hii wahusika ambao wameshughulikiwa ni Paa kutoka katika riwaya ya Nagona na Mzee kutoka katika riwaya ya Mzingile. Uchambuzi umeonesha kuwa utambulisho wa wahusika, Paa na Mzee, umejengwa kupitia uolezi wa mazingira yanayowazunguka, mwonekano wao pamoja na kupitia fikra za wahusika wengine. Kwa ujumla, makala hii imebainisha kuwa uolezi, zaidi ya kuwa mbinu ya kujenga mtazamo kinaratolojia, pia umetumika kujenga utambulisho wa wahusika katika riwaya za Nagona na Mzingile.


Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X