Main Article Content

Matumizi ya kanuni za utambuzi wa mofimu za Nida (1949) katika utambuzi wa mofimu za lugha ya Kiswahili


Elishafati J. Ndumiwe
Tasiana Jasson

Abstract

Utambuzi wa mofimu katika lugha tofautitofauti huongozwa na kanuni za kimajumui zilizopendekezwa na Nida (1949). Kanuni hizo zimehakikiwa katika baadhi ya lugha za Afrikasia ambazo ni Kiyoruba, Kigala na Kihausa. Hata hivyo, kuna utofauti kati ya lugha za Afrikasia na lugha za Kibantu. Isitoshe, kanuni hizo haziko bayana katika lugha za Kibantu. Kwa hiyo, makala hii inahakiki matumizi ya kanuni za utambuzi wa mofimu katika kuchambua mofimu za lugha ya Kiswahili. Data ya makala hii imekusanywa kutoka Kamusi ya Kiswahili Sanifu (2013) kwa kutumia mbinu ya upitiaji wa nyaraka. Aidha, uchambuzi wa data umeongozwa na mkabala wa mofimu kama umbo na maana uliopendekezwa na Rastle na Davis (2008). Matokeo ya makala hii yanaonesha kwamba kanuni tano kati ya sita zinafaa katika kuchambua mofimu za lugha ya Kiswahili. Kanuni hizo ni ya kwanza, ya pili, ya nne, ya tano na ya sita. Kanuni ya tatu haitumiki katika kutambua mofimu za lugha ya Kiswahili kwa sababu maumbo yanayoelezwa na kanuni hii hayamo katika lugha ya Kiswahili kutokana na tofauti za kimuundo kati ya lugha moja na nyingine. Aidha, tumependekeza kuwa uundwaji wa kanuni uendane na maumbo ya lugha tofautitofauti kwa sababu ya umajumui wake.


Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X