Main Article Content

Utoaji Majina ya Mifugo katika Gᴉrᴉmi: Uchunguzi wa Gᴉirwana


Rehema Stephano

Abstract

Makala hii inahusu uchunguzi wa utoaji wa majina ya mifugo katika lugha ya Gᴉrᴉmi, hususani katika lahaja ya Gᴉirwana. Lengo kuu la makala hii ni kubainisha majina pamoja na vigezo vinavyotumika kutoa majina kwa mifugo katika jamii ya Gᴉrᴉmi. Utafiti uliozaa makala hii umetumia mbinu ya usaili katika kukusanya data, ambapo wafugaji kumi (10) wa jamii ya Gᴉirwana kutoka kijiji cha Mpoku kilichopo wilaya ya Singida (Vijijini) walisailiwa. Matokeo yameonesha kuwa vigezo vikuu vinavyotumika katika utoaji wa majina ya mifugo katika Gᴉrᴉmi ni vinne ambavyo ni umri, ujinsi, rangi na dosari. Ng‟ombe huitwa kwa kutumia ujinsi na rangi, dosari (ulemavu), na umri na ujinsi. Mifugo mingine kama mbuzi, kondoo na kuku hutumia umri na ujinsi isipokuwa punda ambaye anatumia kigezo kimoja tu cha umri kwa sababu punda walio wengi wana rangi ya hudhurungi na wachache sana wana rangi nyeupe, na, aghalabu, matumizi makubwa ya punda ni kufanya kazi bila kujali jinsi. Aidha, matokeo ya utafiti yameonesha kuwa katika hatua ya kuzaliwa, mifugo mingi huwa na majina yanayofanana. Majina huanza kugawanywa kwa kuzingatia ujinsi katika hatua ya pili. Makala hii inapendekeza uchunguzi zaidi wa utoaji wa majina ya mifugo kuendelea kufanyika ili kuimarisha mawasiliano katika jamii mbalimbali za wafugaji na kuyahifadhi majina hayo kwa ajili ya vizazi vijavyo.


Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X