Main Article Content
Uhusiano Baina ya Silika na Utendaji wa Wahusika Wakuu wa Fasihi ya Watoto
Abstract
Makala hii inahusu uhusiano baina ya silika na utendaji wa wahusika wakuu wa fasihi ya watoto kwa kurejelea riwaya ya Ngoma ya Mianzi. Data za msingi zilizotumika katika makala hii zilipatikana maktabani kwa kutumia mbinu ya usomaji makini. Nadharia ya Saikochanganuzi imetumika katika ufafanuzi huo, ambayo iliasisiwa na mwanasaikolojia wa Kiswisi Sigmund Freud (1856-1939). Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa kila mhusika ana silika yake yenye sifa zinazomtofautisha na mhusika mwingine. Silika humsukuma mhusika kutenda mambo mbalimbali ambayo yanaweza kuwa hasi au chanya. Hakuna silika bora kuliko nyingine, zote zipo ili kuifanya dunia iwe mahali salama pa kuishi. Mtafiti anaamini kuwa makala hii itakuwa chachu kwa waandishi na watunzi kutunga kazi zitakazoendana na silika za watoto, hivyo, zitakuwa rahisi kueleweka kwa watoto ambao ndio walengwa wakuu. Makala inahitimisha kuwa kuna uhusiano mkubwa baina ya silika na utendaji kwani dhana hizi zinaathiriana na kukamilishana. Silika ndiyo humsukuma mhusika kutenda jambo fulani na huwezi kugundua silika ya mhusika kama hajatenda jambo hilo.