Main Article Content

Itikadi kama Kipengele cha Kimaudhui: Changamoto za Uhakiki na Utatuzi wake


Wallace Kapele Mlaga

Abstract

Lengo la makala hii ni kutatua changamoto zinazojitokeza katika kuihakiki itikadi kama kipengele kimojawapo cha kimaudhui katika matini za kifasihi. Nadharia iliyoongoza utafiti uliozaa makala hii ni Uhistoria Mpya. Kupitia nadharia hii, tunashikilia mwelekeo unaoitazama kazi yoyote ya fasihi kuwa ni chombo cha kiitikadi. Kwa kuwa utafiti wetu ni wa kitaamuli, mbinu ya ukusanyaji data iliyotumika ni udurusu wa mapitio ya maandiko. Aidha, uchanganuzi wa data uliegemezwa katika ruwaza za dhamira zilizojitokeza katika data zetu. Hivyo basi, matokeo ya utafiti huu yamebainisha kwamba sababu za kuwapo kwa changamoto za kuihakiki itikadi kama kipengele cha kimaudhui ni pamoja na mitazamo tofauti kuhusu itikadi katika vipindi tofauti vya wakati, kushikiliwa kwa mtazamo mmoja tu wa itikadi huku mitazamo mingine ikipuuzwa, itikadi kutazamwa kama iliyopoteza umuhimu, na mwisho ni kukosekana kwa mwongozo bayana wa kinadharia wa uchambuzi na ubainishaji wa itikadi katika matini za kifasihi. Suluhisho la changamoto zilizopo ni pamoja na kuifahamu vyema mitazamo yote minne kuhusu itikadi badala ya kushikilia mtazamo mmoja tu. Hii itasaidia kuweza kubaini siyo tu mdhihiriko wa itikadi katika maumbo yake mbalimbali bali pia kuachana na mitazamo potofu kuhusu itikadi. Aidha, makala inabainisha pia umuhimu wa itikadi kwa mtu binafsi au kundi la kijamii katika karne ya ishirini na moja. Hatimaye, makala inahitimisha kwa kutanabahisha kuwa itikadi inaweza kubainishwa kwa kutumia seti tano za elementi zinazohusiana au kwa kujiegemeza katika usawiri wa makundi kinzani katika matini za kifasihi.


Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X