Main Article Content
Uchambuzi wa Dhima ya Msimulizi katika Bunilizi ya Watoto ya Zindera (2008)
Abstract
Lengo la makala hii ni kuchambua dhima za msimulizi wa hadithi ya ualbino katika bunilizi ya watoto ya Zindera (2008). Msimulizi wa kazi hii anasawiri mitazamo miwili iliyopo katika jamii kuhusu watu wenye ualbino, mitazamo ambayo kwa namna fulani inaelekeana japokuwa inatofautiana. Mtazamo wa kwanza ni wa kizamani ambao unadhihirishwa na watu wa jamii ya Zindera ambao wanawaua watoto wenye ualbino ili kuondoa mikosi, majanga na vifo katika jamii. Mtazamo wa pili unahusisha mauaji au ukataji wa viungo vya watu wenye ualbino kwa ajili ya kutafuta utajiri na kupanda cheo. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni Naratolojia ambayo kwa mujibu wa Bal (2008) inahusu usimulizi wa hadithi. Matokeo ya uchambuzi yanaonesha kuwa msimulizi amejitokeza katika dhima ya usimulizi, mawasiliano, ukosoaji na itikadi. Dhima hizi si ngeni katika fasihi mbalimbali duniani kwani pia zinajitokeza katika fasihi za Wamarekani na Waingereza kwa kutaja kwa uchache.