Main Article Content
Tathmini ya Dosari Zifanywazo na Jamii ya Wairaki katika Ujifunzaji wa Kiswahili
Abstract
Makala hii imechunguza dosari zinazofanywa na wajifunzaji wa Kiswahili katika jamii ya Wairaki kisha kufanya tathmini kuonesha dosari
zinazojitokeza kwa kiwango cha juu zaidi zikilinganishwa na nyingine. Data iliyochunguzwa ni sehemu ya data iliyokusanywa mwezi Januari 2017 kutoka wilaya ya Mbulu katika kata za Kainam, Nahhasey na Murray kwa ajili ya tasinifu ya uzamivu. Data hiyo imekusanywa kwa njia ya insha, ushuhudiaji, hadithi, hojaji na usaili. Uchanganuzi wa data umeongozwa na Nadhariatete Kikwazo. Matokeo ya uchunguzi huu yamebainisha kwamba zipo dosari mbalimbali zinazofanywa na wajifunzaji wa Kiswahili wa jamii ya Wairaki zikiwamo: upatanisho wa kisarufi, udondoshaji na upachikaji wa viambishi. Aidha, matokeo yamebaini zaidi kwamba dosari za upatanisho wa kisarufi ambazo zinajidhihirisha katika kipengele cha sintaksia ndizo zinazojitokeza kwa kiwango cha juu ikilinganishwa na nyingine kwa wajifunzaji hao. Matokeo ya makala hii yamehitimisha kwamba ni dhahiri kuwa ujifunzaji wa lugha zilizo katika mnasaba tofauti zinahusisha ufanyaji zaidi wa dosari kama ilivyobainika kwa wajifunzaji hawa. Hii ni kwa sababu kipengele cha upatanisho wa kisarufi kinabeba mawanda mapana ya kimawasiliano kilinganisha na vipengele vya sauti na njeo vilivyobainishwa na watafiti wengine.