Main Article Content
Dhima ya Taswira katika Ufasiri na Uteguzi wa Vitendawili
Abstract
Vitendawili ni utanzu wa fasihi simulizi ambao umechunguzwa kwa kiasi kikubwa hasa kuhusu maana, muundo pamoja na dhima zake. Aidha, imedhihirika kuwa utanzu huu ni tajiri katika matumizi ya lugha ya picha na ishara ambazo hufumbata sitiari inayotarajiwa kufumbuliwa. Hata hivyo, namna ambavyo picha na ishara hizo hufasiriwa na kupata maana bado haijachunguzwa. Katika makala hii tumebainisha namna taswira zinavyowezesha vitendawili kueleweka kwa kurahisisha tafsiri ya picha zilizotumika, kuondoa utata, kutumia maneno kiiktisadi, na hivyo, kuwezesha hadhira kufumbua kitendawili kwa wepesi na kuuona ulimwengu wake kwa upya. Data za makala hii zilipatikana kwa njia ya uchunguzi matini, mahojiano na mjadala wa vikundi baina ya mtafiti na watoataarifa wake kutoka baadhi ya mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani. Imebainika kwamba taswira katika vitendawili ina dhima kadhaa katika ufasiri na uteguaji wa vitendawili hivyo, ikiwamo kuondoa utata, kuutazama ulimwengu upya na kuleta iktisadi.