Main Article Content

Riwaya ya Walenisi na Uhalisi Wake katika Nchi Zinazoendelea


Gerephace Mwangosi

Abstract

Wanafasihi wanatumia mbinu za kisanii kuelezea masuala mbalimbali yanayosawiri hali halisi katika jamii zao. Miongoni mwa masuala yanayoelezwa ni athari za ukoloni mamboleo, ukosefu wa haki, uongozi mbovu pamoja na matabaka yaliyotamalaki katika jamii. Makala hii inajaribu kuelezea mchango wa dhamira za fasihi ya Kiswahili katika kujadili hali halisi ya maisha ya kila siku ya jamii hasa katika kipindi hiki cha sera za soko huria katika nchi zinazoendelea. Kwa kurejelea riwaya ya Walenisi ya Katama Mkangi (1995), makala inatalii hali halisi ya nchi zanazoendelea katika kipindi hiki ambapo hali ya uchumi, siasa na utamaduni, kwa kiasi kikubwa, inadhibitiwa na ubepari na mataifa yaliyoendelea. Aidha, makala inadokeza hali halisi, mwelekeo na matokeo ya sasa na yajayo katika nchi zinazoendelea. Data za makala hii zimepatikana kwa kusoma riwaya ya Walenisi na nyaraka nyinginezo. Nadharia ya Uhalisia imetumika katika uchambuzi wa data. Makala inahitimisha kwamba kadiri mataifa ya kibepari yanavyotumia mbinu za hali ya juu kuhakikisha masilahi yao yanatimizwa, ndivyo uchumi katika nchi zinazoendelea, zikiwamo za Afrika Mashariki, unavyozidi kudhoofika na kuporomoka.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X