Main Article Content
Wasifu wa Mwanamiti
Abstract
Utungo huu umetungwa kwa heshima ya marehemu Profesa Wangari Maathai, mama mtunza mazingira, aliyejitolea kwa hali na mali kutetea haki, usawa wa jinsi, amani, demokrasia na umoja wa taifa la Kenya. Mama huyo alikuwa mwanamke wa kwanza nchini Kenya kupata shahada ya uzamivu akiwa na umri wa miaka thelathini. Alikuwa mwanamke wa kipekee katika usomi, uhadhiri, utafiti na kamanda mkuu wa jeshi la walinda mazingira. Profesa Wangari, kama tulivyomjua, alikuwa mwanamke wa kwanza barani Afrika kutunukiwa Tunzo ya Amani ya Nobel mwaka 2005 kwa kutambua mchango wake adhimu kwa kuzilinda rasilimali za taifa kupitia kuihamasisha jamii mashinani kuishi kwa amani na kuhifadhi mazingira. Kutokana na upendo mkubwa niliokuwa nao kwake, moyo wangu ulifumwa mkuki mkali kwa mauko yake. Ilivyo desturi ya jamii yangu katika maombolezi, nilijikuta nikimlilia huku nikimnuizia maneno mengi. Kilio changu kikageuka kuwa Wasifu wa Mwanamiti.