Main Article Content

Taswira ya Utandawazi katika Riwaya Mpya ya Kiswahili: Mfano wa Riwaya ya Dunia Yao


Alex Umbima Kevogo

Abstract

Nyenzo kuu za kuenezea utandawazi ni lugha, fasihi yake, vyombo vya habari, muziki na tafsiri. Tunapozungumzia utandawazi tunazungumzia maisha yetu ya kila siku na lugha tunayoitumia katika elimu, mawasiliano na mazungumzo. Kwa upande mwingine, utandawazi ni mfumo wa kimataifa unaorahisisha mawasiliano na mahusiano katika nyanja za kiuchumi, kibiashara, na kisiasa uliojikita kwenye maendeleo ya teknolojia ya habari. Kwa hivyo lugha ya Kiswahili pamoja na fasihi yake ni nyenzo muhimu ya kuenezea utandawazi. Makala hii inahoji kuwa uchumi, biashara na siasa ni asasi muhimu ambazo huathiri maendeleo ya jamii. Taathira za asasi hizi hujitokeza katika lugha inayotumiwa kila siku katika elimu, mawasiliano, mazungumzo na fasihi. Matumizi haya ya lugha kimaandishi au kimazungumzo hudhihirika katika muktadha maalum wa utamaduni na mazingira ya jamii husika. Jamii imekubali mabadiliko ya sayansi na teknolojia na kuuruhusu uhusiano baina ya wanajamii uwe umeelekezwa kwenye fikra za maendeleo haya. Kwa hiyo, uhusiano wa fasihi na utamaduni wa jamii umekuzwa chini ya misingi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia ambayo yamemtoa mwanajamii nje ya mipaka ya fikra finyu za utamaduni wake tu hadi ule wa kimataifa. Lugha inayotumiwa katika kazi fulani ya fasihi huathiriwa na kile kinachotokea katika jamii ya mwandishi. Mwandishi huchota fikra, maudhui, falsafa, itikadi, mtindo, maumbo na miundo lugha kutoka kwenye jamii hiyo hasa inapokuwa katika kasi ya mabadiliko. Lengo la makala hii ni kutathmini hali hii inavyojitokeza katika fasihi ya Kiswahili kwa kutumia mfano wa riwaya ya Dunia Yao ya S.A. Mohamed (2006).

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X