Main Article Content

Dhima za Mbinu Linganishi katika Kuhusisha Lugha na Lahaja


Pendo Mwashota

Abstract

Lengo la makala hii ni kujadili dhima za Mbinu Linganishi katika kuhusisha lugha na lahaja. Data za makala hii zilikusanywa kwa kutumia mbinu mbalimbali ambazo ni usaili, ushuhudiaji, hojaji na majadiliano katika majopo. Utafiti ulifanyika Tanzania Bara hususan Mkoani Mtwara na Tanzania Visiwani katika maeneo ya Pemba na Unguja. Utafiti umeongozwa na Nadharia ya Isimu Historia-Linganishi iliyoasisiwa na William Jones (1786). Katika makala hii nadharia hii imetumika kwa sababu suala linalozungumziwa linahusu Mbinu Linganishi hususan dhima zake katika kuhusisha lugha na lahaja. Matokeo ya utafiti wa makala hii yamebaini kuwa Mbinu Linganishi ina dhima mbalimbali katika suala zima la uhusiano baina ya lugha na lugha, na lugha na lahaja. Mbali na dhima hizo makala imebaini kuwa mbinu hiyo ina mipaka mbalimbali ambayo haina budi kuzingatiwa wakati wa kuhusianisha lugha au lahaja. Hii inatokana na kwamba wanaisimu wengi wamejikita katika kulinganisha lugha za Kibantu na Kiswahili huku wakisahau lahaja za lugha za Kibantu ambazo baadhi ya wanaisimu kama vile MLUTA (2009) wameziainisha kama lugha kamili ilhali baadhi ya wanaisimu kama vile Kraal (2005) na Amani (2010) wanazichukulia kama lahaja1. Makala hii imeweka bayana kuwa ni vema ulinganishi wa lugha za Kibantu na lahaja zake ukachukuliwa kwa umakini mkubwa kwa sababu haitoshi kutoa mahitimisho yasiyo na uthibitisho kuwa lugha fulani zipo katika kundi moja ilhali zinatofautiana. Pia, imependekezwa kuwa ipo haja ya kufanya uchunguzi wa kina wa lugha za Kibantu na lahaja zake kwa kutumia Mbinu Linganishi ili kuibuka na matokeo toshelevu yatakayotuwezesha kuainisha vema lugha za Kibantu na lahaja zake2.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X