Main Article Content

Mbinu za Utunzi wa Nyimbo za Uganga wa Pepo Zanzibar: Mifano kutoka Jamii ya Watumbatu


Hassan Gora Haji

Abstract

Miongoni mwa amali za kijadi za Wazanzibari ni uganga wa pepo (uganga wa shetani). Katika kila kijiji cha Zanzibar hakosekani mganga wa asili. Mganga huyo anaweza kuwa wa mitishamba, mahirizi, makafara, zinguo au pungwa kama komero, rubamba, puuwo na umundi. Katika makala hii tunazungumzia mtindo wa nyimbo za uganga wa pepo – mbinu za utunzi (nyimbo hizi hutungwaje?) hususan katika jamii ya Watumbatu. Waganga wa pepo mara nyingi hutumia nyimbo wakati wa kupunga ili kunogesha uganga na kurahisisha pepo wa muwele apande kichwani kwa haraka kwani inadhaniwa kuwa pepo nao pia wanapenda muziki na nyimbo. Kwa hivyo, wanapoimbiwa hupanda kichwani mara moja bila ya kuchelewa. Nyimbo za uganga wa pepo zimegawanyika katika makundi mawili: nyimbo zinazofuata kaida za ushairi wa kimapokeo, na nyimbo zisizofuata kaida za arudhi. Mara nyingine nyimbo za uganga wa pepo huimbwa kufuatana na matukio ya uganga wenyewe unavyofanywa. Makala hii basi inalenga kuzichunguza nyimbo hizo hususani mbinu zake za utunzi. Utafiti wetu umebaini kuwa nyimbo hizo hutumia mbinu mbalimbali katika utunzi wake.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X