Main Article Content
Mbinu za Utunzi wa Nyimbo Ndefu katika Ngoma ya Wigashe
Abstract
Wamitila (2003) anasema kuwa utunzi wa nyimbo zote huongozwa na mbinu na kanuni mbalimbali. Sifa ya idadi ya mistari huchukuliwa kama kanuni (Shitemi, 2010). Hata hivyo, katika jamii za Wasukuma, nyimbo ndefu za Wigashe ziitwazo Busoloja (Makoye, 2010) au Maliliko (Gunderson, 1999) zinazoimbwa kwa mfululizo kwa dakika 30 hadi 180 si za kawaida kutokana na urefu wake, zikilinganishwa na nyimbo nyingine zilizozoeleka. Tafiti zilizotangulia zinaeleza tu kuwa mbinu zinazotumiwa na manju katika utunzi wa nyimbo ndefu za Wigashe ni urudiaji usio wa kawaida (Mkongola, 1980) na kuzifanya zitumie muda mrefu yaani dakika 30 hadi 180 (Makoye, 2010). Makala haya yanabainisha mbinu za utunzi wa nyimbo ndefu za ngoma hiyo ya Wigashe, ya jamii ya Wasukuma ili kuongeza welewa kwa wanataaluma katika fasihi simulizi.