Main Article Content
Usimulizi katika Utenzi wa Swifa ya Nguvumali
Abstract
Makala haya yanachunguza usimulizi katika Utenzi wa Swifa ya Nguvumali uliotungwa na Hassan bin Ismail. Yanachunguza jinsi fani ya usimulizi, iliyodaiwa na wahakiki wa ushairi wa Kiswahili kuupa utenzi huu upekee, ilivyotumiwa na mtunzi ili kufanikisha uwasilishaji wa ujumbe husika. Mambo ambayo tumedhamiria kuyachunguza ni yale yanayohusiana na usimulizi kama vile maudhui (yanayosimuliwa), msimulizi, aina za usimulizi, na maajenti wa usimulizi. Makala haya yana sehemu tatu; sehemu ya kwanza ni utangulizi unaofafanua usuli wa mada ya utafiti na madhumuni ya utafiti, sehemu ya pili inaonesha nadharia iliyoongoza utafiti na sehemu ya tatu ni matokeo ya utafiti na hitimisho. Huu ni utafiti wa kifasihi ambao umefanyiwa maktabani kwa kusoma, kuchambua na kuhakiki matini ya utenzi na kuwasilisha matokeo ya uchunguzi.