Main Article Content

Nafasi ya Lugha na Vyombo vingine vya Kimawasiliano katika Vita Dhidi ya UKIMWI Nchini Kenya


Mosol Kandagor

Abstract

Zaidi ya miongo mitatu iliyopita masuala ya UKIMWI1 yalianza kuripotiwa ulimwenguni. UKIMWI ni mojawapo ya magonjwa ambayo hayana tiba na kwamba umeenea kwa kasi sana katika mataifa mbalimbali ulimwenguni. Mataifa mengi ulimwenguni yameendelea kutatizika kutokana na athari za ugonjwa huu. Kwa mfano, nchini Kenya UKIMWI umewaangamiza watu wengi, na kwa sasa ni janga la kitaifa; ugonjwa huo ulitangazwa kuwa janga la kitaifa mwaka 1999. Makala haya basi yanabainisha nafasi ya lugha na vyombo vingine vya kimawasiliano katika kukabiliana na UKIMWI. Aidha, makala yanajikita katika kuonyesha jinsi wahudumu wa Wizara ya Afya pamoja na wadau wengine wanavyoteua na kutumia istilahi maalumu katika harakati za kupunguza kuenea kwa ugonjwa huu ambao kwa hakika hukita mizizi kila uchao. Utafiti huu ulifanywa katika taasisi mbalimbali zinazohusika na utafiti wa UKIMWI na pia wagonjwa wenyewe kwa kutathmini nafasi ya lugha katika harakati zao za kukabiliana na ugonjwa huo. Data zilizochanganuliwa zilikusanywa kutoka kituo cha AMPATH2-Eldoret, mabango, vyombo vya habari na maandishi mengine yanayobeba maelezo juu ya kupunguza kuenea kwa UKIMWI.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X