Main Article Content

Msigano wa Majina ya ‘Walemavu’ katika Jamii ya Wazungumzaji Kiswahili: Mifano kutoka Tanzania


Elizabeth G. Mahenge

Abstract

Walemavu wamekuwa wakilalamikia matumizi ya majina yanayowarejelea katika jamii ya wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili. Jambo hili nililigundua wakati nilipokuwa ninafuatilia vipindi vya walemavu katika runinga na redio nchini Tanzania. Majina kama vile kilema, kiwete, kipofu, zeruzeru, asiyesikia na mengineyo ni baadhi ya majina ambayo wazungumzaji wamekuwa wakiyatumia kwa muda mrefu (yaani tangu zamani za kale) lakini kwa upande mwingine wanaoitwa majina hayo wamekuwa wakiyakataa. Makala haya yanachunguza msigano wa majina wanayoitwa ‘walemavu’ nchini Tanzania. Vilevile, makala yatazungumzia vikwazo mbalimbali wanavyokutana navyo walemavu katika mawasiliano. Mambo haya yana umuhimu mkubwa wa kuzungumziwa katika makala haya kwani lengo kuu la kuwepo kwa ‘lugha’ katika jamii ni mawasiliano. Pia makala haya yatatoa mapendekezo mbalimbali kuhusiana na mambo ambayo yameshughulikiwa katika utafiti huu.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X