Journal of Kiswahili and Other African Languages https://www.ajol.info/index.php/jkal
The Journal of Kiswahili and Other African Languages is a high quality open-access, peer-reviewed and refereed multidisciplinary research journal, dedicated to serve the society by the global dissemination of information through an unparalleled commitment to quality, reliability, and innovation and research work. Journal of Kiswahili and Other African Languages welcomes and acknowledges high quality theoretical and empirical original research papers, case studies, review papers, literature reviews and conceptual framework from researchers, academicians, professional, practitioners and students from all over the world. Journal of Kiswahili and Other African Languages engages its noble efforts for the development and endeavours to give you the best.

You can view this journal's website here.
Utafiti Foundation en-US Journal of Kiswahili and Other African Languages 2958-4914 Mkakati wa Tafsiri Mkopo wa Istilahi za Kiingereza katika Kiswahili na Athari zake: Uchanganuzi wa Vidahizo Teule vya Kamusi ya Biolojia, Fizikia na Kemia https://www.ajol.info/index.php/jkal/article/view/267585
Makala hii inachunguza mkakati wa tafsiri mkopo wa istilahi za Kiingereza katika Kiswahili na athari zake kwa kuangazia uga wa biolojia,  fizikia na kemia kupitia vidahizo teule vya Kamusi ya Biolojia, Fizikia na kemia (2012). Azma kuu ya uchunguzi huu ni kutathmini mchango  wa tafsiri mkopo wa msamiati wa Kiingereza katika suala zima la kukuza lugha ya Kiswahili. Kwa mujibu wa makala hii eneo hili  halijapewa aula miongoni mwa mada mbalimbali za tafsiri zilizokwishachunguzwa. Hii imemuhamasisha mtafiti kulishughulikia eneo hili.  Data ya makala hii ilikusanywa uwandani katika idara na taasisi zilizo katika jiji la Dar es Salaam kwa njia ya usaili, hojaji na chanzo cha  data cha maktabani. Idara na taasisi zilizohusishwa katika ukusanyaji wa data ni: Idara ya Lugha za Kigeni na Isimu, TATAKI kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na BAKIZA. Idara na taasisi hizi zinapatikana mkoani Dar es Salaam Wilaya ya Ubungo ambapo mtafiti  alifanikiwa kudodosa na kufanya mahojiano ya ana kwa ana kwa wataalamu wa tafsiri. Aidha, data ilikusanywa kutoka katika matini  mbalimbali kutoka chanzo cha data cha maktabani. Mathalani, kamusi, tasinifu, majarida na vitabu kadhaa kulingana na mada ya makala  hii. Malengo ya makala hii yametimizwa kwa kuongozwa na Nadharia ya Istilahi za Kisayansi iliyoasisiwa na Kiingi (1989) na kuendelezwa  na Kiingi (1992) na Kiingi (1998) na Mwaro-Were (2000, 2001). Halikadhalika, data ya makala hii imechambuliwa kwa kutumia mkabala wa  maelezo. Aidha, matokeo yameonesha kuwa Kiswahili kimejipatia istilahi lukuki katika tasnia ya biolojia, fizikia pamoja na kemia kupitia  mkakati wa tafsiri mkopo. Makala hii ni muhimu kwa wanaisimu kwani inabainisha istilahi mbalimbali za lugha ya Kiingereza katika  uwanja wa biolojia, fizikia pamoja na kemia zilizoingizwa katika Kiswahili kupitia tafsiri mkopo. Inapendekezwa kuwa watafiti wa lugha  wachunguze njia nyinginezo za ukopaji zinazokiendeleza Kiswahili kama vile utohozi na uasilishaji.
Editha Adolph Simon Chipanda Copyright (c) 2024 https://creativecommons.org/licenses/by-nc-sa/4.0 2024-03-27 2024-03-27 2 1 1 9 Uchopekaji wa Vipande vya Simulizi katika Riwaya za S. A. Mohamed, Dunia Yao (2006) na Nyuso na Mwanamke (2010) https://www.ajol.info/index.php/jkal/article/view/267587
Makala haya yanachunguza matumizi ya uchopekaji wa vipande vya simulizi katika riwaya mbili za S. A. Mohamed, Dunia Yao (2006) na  Nyuso za Mwanamke (2010). Uchunguzi huu uliongozwa na Nadharia ya Ubaadausasa ambayo hupendekeza uanuwai wa mawazo kwa  kukaidi kuwepo na mtazamo mmoja wa kueleza ulimwengu na tajriba za binadamu, au simulizi kuu. Uchanganuzi umedhihirisha kuwa mwandishi wa riwaya hizi alitumia kimakusudi vipengele vya kibaadausasa ili kukaidi simulizi kuu zilizotawala. Riwaya hizi zilitumia  uchopekaji wa vipande vya simulizi kuvuruga urazini, mshikamano, na muumano wa usimulizi wa riwaya za kimapokeo. Kimaudhui,  riwaya hizi zinasaili mwelekeo chanya uliohusishwa na uhuru. Zinaonyesha kuwa mataifa mengi ya Afrika yametawaliwa na hali ya  utamauishi baada ya uhuru. Vilevile, misaada inayotolewa na mataifa ya ulaya hutumika kama chambo cha kueneza ukoloni mamboleo  katika mataifa ya Afrika. Hali kadhalika, riwaya hizi zinaonyesha changamoto ambazo wahamiaji hupitia wanapohamia ughaibuni  kutafuta maisha bora. Ni bayana kuwa mwandishi wa riwaya hizi ametumia mtindo wa uandishi wa ubaadausasa kama mbinu ya kiumbuji inayokaidi uandishi wa kimapokeo. Vilevile, riwaya hizi zimetumika kudhihirisha fujo, ghasia, na ukosefu wa mshikamano katika  ulimwengu wa karne ya ishirini na moja.
Mary Njambi Muigai Issa Mwamzandi Robert Oduori Copyright (c) 2024 https://creativecommons.org/licenses/by-nc-sa/4.0 2024-03-27 2024-03-27 2 1 10 19 Uamilifu wa Ngazi ya Utambuzi katika Riwaya Teule za Kiswahili https://www.ajol.info/index.php/jkal/article/view/267588
Makala haya yanachunguza ngazi ya utambuzi na uamilifu wake katika riwaya za Kiswahili zilizoteuliwa makusudi kwa uchunguzi huu.  Riwaya hizo ni; Nyuso za Mwanamke (S. Mohamed, 2010), Harufu ya Mapera (K. Wamitila, 2012), Hujafa Hujaumbika (F. Kagwa, 2018),  Haini (A. Shafi, 2002), na Ndoto ya Almasi (K. Walibora, 2006). Ngazi ya utambuzi ni mojawapo ya ngazi mbalimbali za ufokasi  zilizopendekezwa na wananaratolojia. Kimsingi, ufokasi ni mtazamo ambao huchukuliwa katika kuwasilisha simulizi na kuikuza hadithi kwa ujumla. Data ya kuudhibiti na kuthibitisha madai ya mjadala wetu imetolewa katika riwaya teule. Uteuzi wa riwaya hizi unahalalishwa  kwa misingi kwamba, hizi ni riwaya zilizo na matini pana zinazowezesha udondoaji wa mifano faafu inayodhihirisha ngazi  za ufokasi na wakati huo huo kudhihirisha uamilifu wa ngazi hizo katika simulizi. Mjadala wa kimsingi katika makala haya umekitwa na  kuongozwa na madai ya teneti za kimsingi za nadharia ya naratolojia ambayo inatambua ufokasi na uhusika kama vipengele muhimu  katika uwasilishaji wa simulizi.
Dinah Sungu Osango Mwenda Mbatiah Rayya Timammy Copyright (c) 2024 https://creativecommons.org/licenses/by-nc-sa/4.0 2024-03-27 2024-03-27 2 1 20 30 Mtazamo wa Ki-Afrika katika Nadharia za Tafsiri https://www.ajol.info/index.php/jkal/article/view/274797
Makala haya yanahusu Mtazamo wa Ki-Afrika katika Nadharia za Tafsiri. Inafahamika kuwa chimbuko la nadharia za tafsiri zilizopo ni nchi  za Kimagharibi. Hata hivyo, katika nchi za Afrika taaluma ya tafsiri imepiga hatua kubwa ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuwa na  wataalamu na wanataaluma wengi wa tafsiri, kufundishwa katika shule za sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu. Pamoja na maendeleo  hayo, mpaka sasa hakuna nadharia ya tafsiri iliyobuliwa kupitia mazingira, muktadha na utamaduni wa lugha ya Kiswahili kama lugha ya Ki-Afrika. Hivyo, makala haya yanalenga kujadili umuhimu wa kuunda nadharia za tafsiri kwa kutumia muktadha wa lugha za Ki-Afrika na  kupendekeza hatua zitakazochukuliwa katika mchakato wa kuunda nadharia za tafsiri za Kiswahili. Makala yanajadili kwamba, pamoja na  kuwapo kwa nadharia zilizoibuliwa na wanazuoni wa Kimagharibi, kuna umuhimu wa kuunda nadharia za tafsiri ambazo zimefungamana  na muktadha, mazingira, mila, desturi, historia, lugha na utamaduni wa Ki-Afrika. Hii ni kwa sababu tafsiri hushughulika  na lugha ambayo ni mali ya jamii yenye utamaduni mahususi. Hivyo, nadharia za tafsiri zilizofumbata mtazamo wa Ki-Afrika zitakuwa  msingi, dira na mwongozo wa kinadharia na kivitendo katika kushughulikia tafsiri za matini mbalimbali za lugha za Ki-Afrika, hasa  zinazohusu dhana za kiutamaduni na fasihi. Vilevile nadharia hizo zitakuwa ni suluhisho la matatizo na changamoto za tafsiri kiisimu, kisemantiki, kiutamaduni na kifasihi. Makala haya yanapendekeza kuwa nadharia za tafsiri zinaweza kuundwa kwa kutumia mbinu  mbalimbali kama vile kuunda nadharia mpya, kuasili nadharia zilizopo na kuziboresha nadharia hizo.
Hadija Jilala Copyright (c) 2024 https://creativecommons.org/licenses/by-nc-sa/4.0 2024-07-24 2024-07-24 2 1 31 40 Viashiria vya Kujiua: Uchunguzi wa Mhusika Kazimoto katika Riwaya ya Kichwamaji https://www.ajol.info/index.php/jkal/article/view/274800
Wahusika katika kazi za fasihi huumbwa kwa ustadi mkubwa kwa lengo la kubeba tafakuri na fikra za mtunzi kuhusu maisha ya jamii.  Katika uumbaji huo, aghalabu, binadamu husawiriwa kama kiumbe anayeteseka na anayeishi katika ulimwengu usiomjali, aliyezungukwa  na mateso na ubwege1, na anayeshindwa kukabiliana vyema na uhalisia wake (Wamitila, 2002). Mambo hayo, ndiyo  huweza kusababisha afanye maamuzi fulani kama vile kujiua. Hivi ndivyo anavyofanya Euphrase Kezilahabi katika riwaya ya Kichwamaji  (1974) anapomuumba mhusika anayejiua. Hata hivyo, kwa kuwa kujiua huambatana na viashiria mbalimbali, makala haya yanajadili  viashiria vya kujiua kwa mhusika mkuu katika riwaya teule tu. Riwaya hiyo imeteuliwa kwa sababu ina mawanda ya kutosha  yaliyowezesha kupata data zilizolengwa katika makala haya. Pia, riwaya hiyo imeteuliwa kama sampuli ya kuwakilisha riwaya nyingine  zenye viashiria vya kujiua. Misingi ya Nadharia ya Udhanaishi imetumika katika uchunguzi, uchanganuzi na uwasilishaji wa matokeo. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya uchambuzi wa matini. Mjadala umebainisha kwamba katika riwaya ya Kichwamaji vipo viashiria vinne  vya kujiua vilivyomkumba Kazimoto kabla ya kujiua kwake. Viashiria hivyo ni kukata tamaa, kujitenga kijamii, kuzungumzia  masuala ya kujiua na mabadiliko ya tabia. Makala yanahitimisha kwamba jamii inahitaji kupewa elimu ya kutosha kuhusu kujiua kwa  wahusika pamoja na viashiria vyake ili iweze kumtambua na kumsaidia mtu mwenye viashiria vya kujiua.
Adria Fuluge Copyright (c) 2024 https://creativecommons.org/licenses/by-nc-sa/4.0 2024-07-24 2024-07-24 2 1 41 50