https://www.ajol.info/index.php/jkal/issue/feedJournal of Kiswahili and Other African Languages2025-02-03T15:09:53+00:00Professor Mosol Kandagormosolkandagor@gmail.comOpen Journal Systems
The Journal of Kiswahili and Other African Languages is a high quality open-access, peer-reviewed and refereed multidisciplinary research journal, dedicated to serve the society by the global dissemination of information through an unparalleled commitment to quality, reliability, and innovation and research work. Journal of Kiswahili and Other African Languages welcomes and acknowledges high quality theoretical and empirical original research papers, case studies, review papers, literature reviews and conceptual framework from researchers, academicians, professional, practitioners and students from all over the world. Journal of Kiswahili and Other African Languages engages its noble efforts for the development and endeavours to give you the best.

You can view this journal's website here.
https://www.ajol.info/index.php/jkal/article/view/288170Tathmini ya Matumizi ya Akili Unde Kama Nyenzo ya Kutafsiri Matini za Kiingereza Kwenda Kiswahili2025-02-03T13:47:49+00:00Hadija Jilalamosolkandagor@gmail.com
Dhana ya akili unde au akili bandia inarejelea mwigo au ukadiriaji wa akili ya binadamu katika mashine. Lengo la akili unde ni pamoja na matumizi ya kompyuta yaliyoboreshwa kuhoji na kutambua mambo anuwai unde na ya tasnia mbalimbali (Jurafsky na Martin, 2020). Makala hii inalenga kutathmini matumizi ya akili unde kama nyenzo ya kutafsiri matini za Kiingereza kwenda Kiswahili. Data ya makala hii imekusanywa maktabani kwa kupitia maandiko na pia uwandani kwa kuwahoji wanataaluma mbalimbali. Uchambuzi na uwasilishaji wa data ya makala hii umeongozwa na Mkabala wa Uchambuzi wa Maudhui ya Krippendorff (2004). Matokeo ya uchunguzi yanaonesha kuwa akili unde ina ubora kwa vile hufanya kazi kwa kasi, gharama ni nafuu, urahisi, kutafsiri lugha nyingi na unyumbufu wa kuunganishwa na teknolojia nyingine. Kwa upande mwingine makala hii imebainisha udhaifu wa matumizi ya akili unde kama vile kutozingatia muktadha, kukosa ubunifu, tofauti za kiisimu, kukosa usalama na upinzani wa wanaisimu. Kutokana na udhaifu huo, Makala hii inapendekeza kuwa uwekwe uangalizi wa binadamu katika mifumo, kushughulikia utata, kuboresha mifumo kila muda, kuwekwe sehemu ya maoni ya mtumiaji na matumizi ya mbinu msetu. Hivyo, ni muhimu kuweka usawa kati ya ufanisi wa mashine na uelewa wa watafsiri wa kibinadamu katika uendelezaji na utekelezaji wa akili unde katika tafsiri.
2025-02-03T00:00:00+00:00Copyright (c) 2025 https://www.ajol.info/index.php/jkal/article/view/288171Epistemolojia ya Waafrika katika Semi Zilizoandikwa kwenye Vazi la Kanga za Waswahili2025-02-03T14:00:38+00:00Martina Duwemosolkandagor@gmail.com
Epistemolojia ya Waafrika, wakiwamo Waswahili hubainika kupitia sanaa inayobeba mitazamo inayozingatiwa katika jamii yao. Moja kati ya mambo yanayobainisha sanaa ya Waswahili ni vazi la kanga. Kwa jumla, usanaa katika vazi hilo hudhihirika kupitia maumbo au michoro na lugha ya kiufundi ambayo hubeba semi kama vile, mafumbo, methali na misemo. Vazi la kanga huthaminiwa na hutumiwa kwa namna mbalimbali katika maisha ya Waswahili, mathalani, kufunga kiunoni, kichwani, kujifunika na kama pambo (Hanby na Bygott, 1984). Kwa jumla, semi zilizoandikwa kwenye vazi la kanga zimefafanuliwa zaidi katika muktadha wa dhamira na dhima pasipo kumakinikiwa kwa kina katika muktadha wa kiepistemolojia kulingana na kaida za Waswahili wenyewe. Makala haya yanafafanua namna semi hizo zinavyobeba na kuhifadhi maarifa ya kiepistemolojia yanayosawiri maisha halisi ya Waswahili. Vilevile, misingi ya Nadharia ya Sosholojia ya Kifasihi imetumika kama mwegamo mkuu katika kuchunguza, kuchanganua na kuwasilisha data husika. Matokeo yanaonesha kuwa maandishi yaliyopo katika vazi la kanga yanahifadhi fasihi ya Waswahili, hususani semi ambazo hubainisha maarifa mbalimbali, yakiwemo ya kiepistemolojia. Hivyo, makala haya yanajadili baadhi ya vipengele hivyo ambavyo ni: maarifa kuhusu kuwapo kwa kani kuu, thamani ya kazi, heshima na utiifu na uvumilivu.
2025-02-03T00:00:00+00:00Copyright (c) 2025 https://www.ajol.info/index.php/jkal/article/view/288172Uamilifu wa Jazanda Kwenye Nyimbo za Kiasili za Kikamba2025-02-03T14:05:08+00:00E.K. Muemosolkandagor@gmail.comM.N. Wafulamosolkandagor@gmail.comR. Oduorimosolkandagor@gmail.comR. Oduorimosolkandagor@gmail.com
Jamii ya Wakamba huwasiliana kwa njia mbalimbali fasihi simulizi ikiwa njia mojawapo. Fasihi simulizi ya Wakamba hujumuisha vipera anuai nyimbo za kiasili zikiwemo. Nyimbo za kiasili ni maarufu na huwasilishwa katika takriban kila shughuli na hafla za kijamii. Kupitia nyimbo hizi, itikadi ya Wakamba huwasilishwa kwa hadhira. Hata hivyo, itikadi hii aghalabu hufumbatwa kijazanda. Makala haya yanatathmini uamilifu wa jazanda mahsusi kifani na kimaudhui kwenye nyimbo za kiasili za Kikamba. Data ya utafiti imechanganuliwa na maelezo kutolewa kulingana na malengo ya utafiti na mihimili ya kinadharia. Nadharia ya Jazanda Dhanifu imeuongoza uhakiki wa data. Data ya kimsingi ilitokana na nyimbo za kiasili za Kikamba zilizokusanywa kutoka Tume ya Permanent Presidential Music Commission nchini Kenya. Nyimbo zilizosheheni jazanda zilisampuliwa kimakusudi. Matokeo ya utafiti huu ni rejeleo muhimu kwa taaluma ya fasihi simulizi ya Kiswahili na lugha nyingine za Kiafrika.
2025-02-03T00:00:00+00:00Copyright (c) 2025 https://www.ajol.info/index.php/jkal/article/view/288173Uhakiki wa Itikadi Zilizofumbatwa Kijazanda kwenye Nyimbo za Kiasili za Kikamba2025-02-03T14:20:43+00:00Noluthando A. Hlongwanethandoh@live.co.zaKarishma Lowtonthandoh@live.co.za
Makala haya yanachunguza itikadi zilizofumbatwa kijazanda katika nyimbo za kiasili za Kikamba. Lengo kuu la makala ni kuhakiki itikadi za Wakamba zinazofumbatwa kijazanda kwenye nyimbo teule. Uchunguzi huu ni wa kithamano. Mbinu ya kimaelezo ilitumika katika ukusanyaji na uchanganuzi wa data. Data ya kimsingi ilitokana na nyimbo nane za kiasili za Kikamba zinazosheheni jazanda. Nyimbo zenyewe zilikusanywa kutoka Tume ya Permanent Presidential Music Commission nchini Kenya. Uteuzi huo ulifanyika kimaksudi kwa maana utafiti ulilenga kuhakiki itikadi zinazofumbatwa kijazanda kwenye nyimbo teule. Data ya uchunguzi huu imechanganuliwa na maelezo kutolewa kulingana na lengo la utafiti na mihimili ya kinadharia. Utafiti umeongozwa na Nadharia ya Jazanda Dhanifu na ile ya Itikadi. Kimsingi, huu ni utafiti wa maktabani kwa kuwa data muhimu zilitokana na rekodi zilizowekwa. Matokeo ya utafiti yalibainisha kuwa nyimbo za kiasili za Kikamba huwasilisha itikadi za Wakamba zilizofumbatwa kijazanda. Itikadi zenyewe zimejikita katika masuala kama vile tohara, kazi, ndoa na mapenzi, ubikira, utamaduni, malezi na mauti. Matokeo ya utafiti huu yanakuza maarifa kuhusiana na dhima ya kipera cha nyimbo katika fasihi simulizi za Kiafrika. Makala haya yanapendekeza kwamba ufasiri wa jazanda kwa mujibu wa nadharia ya Udenguzi ufanywe ili kubaini fasiri mbalimbali kwa mujibu wa hadhira.
2025-02-03T00:00:00+00:00Copyright (c) 2025 https://www.ajol.info/index.php/jkal/article/view/288174Digitising Kiswahili for Translation Economy2025-02-03T14:39:32+00:00K.N. Sangilimosolkandagor@gmail.com
Translation currently is one of the biggest currency earners globally whose net worth stands in billions of US Dollars. Perhaps, when compared to teaching, translation becomes the second richest single entity in a pool of Language Service Providers. Kiswahili language, in its quest to be among the top languages globally has embraced translation and increasingly expanding its horizon. This paper therefore purposed to find out the state and quality of online translation tools like google translate as used by Kiswahili clients in translation services. The research methodology used was qualitative. Random sampling technique was used to get sample words, phrases and sentences. The results show that Google Translate has demonstrated excellent translation results when it comes to individual lexemes as compared to phrases and sentences. In some cases, the phrases, especially when used figuratively, has potential to mislead and give birth to spurious translation. The results of this research will go a long way in helping improve online translation from and into Kiswahili hence not only improving Kiswahili but also opening potentialities of other African languages.
2025-02-03T00:00:00+00:00Copyright (c) 2025 https://www.ajol.info/index.php/jkal/article/view/288175Majuto ni Mjukuu: Uchunguzi wa Mhusika Ngoma katika Riwaya ya Ua la Faraja2025-02-03T14:50:11+00:00Adria Fulugemosolkandagor@gmail.com
Maisha ya mtu ni hadithi inayopaswa kusimuliwa ili kutoa mafunzo kwa jamii kuhusu mapito ya mhusika. Hii inatokana na ukweli kwamba kila mtu katika jamii ana mambo mazuri na/au mabaya ya kusimulia yanayohusu mapito ya maisha yake. Yapo masimulizi yanayofurahisha kutokana na matendo ya mhusika na mengine husikitisha kiasi cha kumfanya mhusika kuyajutia maisha yake kutokana na kufanya au kutofanya jambo fulani. Kwa msingi huo, makala hii ililenga kuchunguza methali inayosema “majuto ni mjukuu” kwa kuchunguza maisha ya mhusika Ngoma katika riwaya ya Ua la Faraja (2004). Mhusika huyu ameteuliwa kama kiwakilishi cha wahusika wengi ambao katika maisha yao, walifanya na/au hawakufanya mambo fulani ambapo kutokana na kufanya na/au kutokufanya kwao, kulisababisha majuto katika maisha yao. Pia, riwaya hii imeteuliwa kama sampuli ya riwaya mbalimbali zenye wahusika wenye sifa kama za mhusika Ngoma. Data zilitokana na uchambuzi wa riwaya ya Ua la Faraja. Vilevile, Nadharia ya Uhalisia ilitumika kama mwongozo katika ukusanyaji wa data, uchambuzi na uwasilishaji wa matokeo ya utafiti wa makala hii. Matokeo yanaonesha kwamba ziko sababu kuu nne zilizosababisha Ngoma ayajutie maisha yake. Sababu hizo ni kukosa uaminifu katika ndoa, kuitelekeza familia yake, kuendekeza anasa, na kutowajali ndugu zake.
2025-02-03T00:00:00+00:00Copyright (c) 2025