Main Article Content

Uhakiki wa Itikadi Zilizofumbatwa Kijazanda kwenye Nyimbo za Kiasili za Kikamba


Noluthando A. Hlongwane
Karishma Lowton

Abstract

Makala haya yanachunguza itikadi zilizofumbatwa kijazanda katika nyimbo za kiasili za Kikamba. Lengo kuu la makala ni kuhakiki itikadi  za Wakamba zinazofumbatwa kijazanda kwenye nyimbo teule. Uchunguzi huu ni wa kithamano. Mbinu ya kimaelezo ilitumika katika  ukusanyaji na uchanganuzi wa data. Data ya kimsingi ilitokana na nyimbo nane za kiasili za Kikamba zinazosheheni jazanda. Nyimbo  zenyewe zilikusanywa kutoka Tume ya Permanent Presidential Music Commission nchini Kenya. Uteuzi huo ulifanyika kimaksudi kwa maana utafiti ulilenga kuhakiki itikadi zinazofumbatwa kijazanda kwenye nyimbo teule. Data ya uchunguzi huu imechanganuliwa na  maelezo kutolewa kulingana na lengo la utafiti na mihimili ya kinadharia. Utafiti umeongozwa na Nadharia ya Jazanda Dhanifu na ile ya  Itikadi. Kimsingi, huu ni utafiti wa maktabani kwa kuwa data muhimu zilitokana na rekodi zilizowekwa. Matokeo ya utafiti yalibainisha  kuwa nyimbo za kiasili za Kikamba huwasilisha itikadi za Wakamba zilizofumbatwa kijazanda. Itikadi zenyewe zimejikita katika masuala  kama vile tohara, kazi, ndoa na mapenzi, ubikira, utamaduni, malezi na mauti. Matokeo ya utafiti huu yanakuza maarifa kuhusiana na  dhima ya kipera cha nyimbo katika fasihi simulizi za Kiafrika. Makala haya yanapendekeza kwamba ufasiri wa jazanda kwa mujibu wa  nadharia ya Udenguzi ufanywe ili kubaini fasiri mbalimbali kwa mujibu wa hadhira. 


Journal Identifiers


eISSN: 2958-4914