Main Article Content

Uamilifu wa Jazanda Kwenye Nyimbo za Kiasili za Kikamba


E.K. Mue
M.N. Wafula
R. Oduori
R. Oduori

Abstract

Jamii ya Wakamba huwasiliana kwa njia mbalimbali fasihi simulizi ikiwa njia mojawapo. Fasihi simulizi ya Wakamba hujumuisha vipera  anuai nyimbo za kiasili zikiwemo. Nyimbo za kiasili ni maarufu na huwasilishwa katika takriban kila shughuli na hafla za kijamii. Kupitia  nyimbo hizi, itikadi ya Wakamba huwasilishwa kwa hadhira. Hata hivyo, itikadi hii aghalabu hufumbatwa kijazanda. Makala haya  yanatathmini uamilifu wa jazanda mahsusi kifani na kimaudhui kwenye nyimbo za kiasili za Kikamba. Data ya utafiti imechanganuliwa na  maelezo kutolewa kulingana na malengo ya utafiti na mihimili ya kinadharia. Nadharia ya Jazanda Dhanifu imeuongoza uhakiki wa data.  Data ya kimsingi ilitokana na nyimbo za kiasili za Kikamba zilizokusanywa kutoka Tume ya Permanent Presidential Music Commission nchini  Kenya. Nyimbo zilizosheheni jazanda zilisampuliwa kimakusudi. Matokeo ya utafiti huu ni rejeleo muhimu kwa taaluma ya fasihi simulizi  ya Kiswahili na lugha nyingine za Kiafrika. 


Journal Identifiers


eISSN: 2958-4914