Main Article Content

Uchopekaji wa Vipande vya Simulizi katika Riwaya za S. A. Mohamed, Dunia Yao (2006) na Nyuso na Mwanamke (2010)


Mary Njambi Muigai
Issa Mwamzandi
Robert Oduori

Abstract

Makala haya yanachunguza matumizi ya uchopekaji wa vipande vya simulizi katika riwaya mbili za S. A. Mohamed, Dunia Yao (2006) na  Nyuso za Mwanamke (2010). Uchunguzi huu uliongozwa na Nadharia ya Ubaadausasa ambayo hupendekeza uanuwai wa mawazo kwa  kukaidi kuwepo na mtazamo mmoja wa kueleza ulimwengu na tajriba za binadamu, au simulizi kuu. Uchanganuzi umedhihirisha kuwa mwandishi wa riwaya hizi alitumia kimakusudi vipengele vya kibaadausasa ili kukaidi simulizi kuu zilizotawala. Riwaya hizi zilitumia  uchopekaji wa vipande vya simulizi kuvuruga urazini, mshikamano, na muumano wa usimulizi wa riwaya za kimapokeo. Kimaudhui,  riwaya hizi zinasaili mwelekeo chanya uliohusishwa na uhuru. Zinaonyesha kuwa mataifa mengi ya Afrika yametawaliwa na hali ya  utamauishi baada ya uhuru. Vilevile, misaada inayotolewa na mataifa ya ulaya hutumika kama chambo cha kueneza ukoloni mamboleo  katika mataifa ya Afrika. Hali kadhalika, riwaya hizi zinaonyesha changamoto ambazo wahamiaji hupitia wanapohamia ughaibuni  kutafuta maisha bora. Ni bayana kuwa mwandishi wa riwaya hizi ametumia mtindo wa uandishi wa ubaadausasa kama mbinu ya kiumbuji inayokaidi uandishi wa kimapokeo. Vilevile, riwaya hizi zimetumika kudhihirisha fujo, ghasia, na ukosefu wa mshikamano katika  ulimwengu wa karne ya ishirini na moja.


Journal Identifiers


eISSN: 2958-4914
 
empty cookie