Main Article Content

Ukuzaji na Uenezaji wa Lugha ya Kiswahili katika Karne ya 21 Kupitia Maazimio, Matamko na Ushauri wa Viongozi wa Serikali katika MASIKIDU


Editha Adolph

Abstract

Makala hii inachunguza ukuzaji na uenezaji wa lugha ya Kiswahili katika karne ya 21 kupitia maazimio, matamko fursa na ushauri wa serikali kabla1 na wakati wa MASIKIDU (siku ya maadhimisho ya siku ya Kiswahili duniani). Azma kuu ni kuangazia namna maazimio, fursa, ushauri na matamko mbalimbali yaliyotolewa na viongozi wa serikali katika MASIKIDU yanavyolenga kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili. Ili kutimiza azma hii, mtafiti ametumia hotuba ya Mh. Samia Suluu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais wa Tanzania Mh. Philip Mpango, Mh. Mohamed Mchengerwa waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Adolph Mkenda Waziri wa Elimu nchini Tanzania na ya Mh. Abdulrahman Kinana makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara kama marejeleo ya maazimio, matamko, fursa na ushauri huo. Kimsingi utafiti huu ni wa uwandani. Utafiti huu umetekelezwa kwa mujibu wa mkabala wa maelezo. Mtafiti alikusanya data kwa kutumia mbinu ya ushuhudiaji. Matokeo ya makala hii yanaonesha kuwa viongozi mbalimbali wa Tanzania wametoa maazimio mbalimbali kuhusiana na lugha ya Kiswahili kupitia MASIKIDU. Miongoni mwa maazimio hayo ni:uanzishwaji wa vituo vya kufundishia Kiswahili kwa wageni, kutoa mafunzo kwa wataalamu wa nyanja mbalimbali za Kiswahili, serikali kutekeleza mkakati wa taifa wa kukifanya Kiswahili kijiuze, ushawishi wa nchi nyingine kuingiza Kiswahili katika mitaala yao.. Aidha, viongozi wameelekeza matumizi ya Kiswahili katika: nyaraka za mawasiliano za wizara na idara zake, mikutano, warsha, semina, mijadala ya umma na dhifa, majina ya barabara, mitaa, mabango, fomu za usaili na maelekezo ya matumizi ya dawa zote na bidhaa. Makala hii ni muafaka kwa wazungumzaji na wanaojifunza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya Tanzania kwani inahamasisha juu ya uandishi, tafsiri, ufundishaji na ujifunzaji wa lugha hii sambamba na fursa lukuki zanazotokana nayo. Vilevile inaonesha ni kwa jinsi gani viongozi wa Tanzania walivyo na mapenzi mema kwa lugha hii aushi na adhimu ya Kiswahili ambapo hii ni chachu ya kukua na kuenea lwa lugha hii. Mtafiti anapendekeza tafiti fuatizi zifanyike juu ya maazimio, matamko fursa na ushauri unaotolewa na viongozi mbalimbali kuhusiana na lugha ya Kiswahili sambamba na utekelezwaji wake.


Journal Identifiers


eISSN: 2958-4914
 
empty cookie