Main Article Content

Vyanzo vya Misimu Miongoni mwa Wanafunzi: Uchunguzi Kifani wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam


Editha Adolph

Abstract

Mtafiti wa makala hii anachunguza vyanzo vya misimu kwa wanafunzi katika Kiswahili. Mtafiti ametumia mbinu za hojaji, usaili na uchambuzi wa matini katika suala zima la kutimiza malengo ya makala hii. Kwa kutumia mbinu ya hojaji, mtafiti aligawa hojaji 15 kwa wanachuo 15 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mtafiti pia kwa kutumia mbinu ya usaili, alifanya mahojiano ya ana kwa ana kwa watafitiwa wake ili kupata data stahiki. Aidha, mtafiti alisoma nyaraka zinazohusiana na mada husika kama vile: majarida, kamusi, tasinifu, vitabu mbalimbali na kadhalika. Kwa pamoja mbinu hizi zimekamilishana katika kumpatia mtafiti data faafu na hivyo kutimiza malengo ya makala hii. Makala hii imeongozwa na Nadharia ya Uchanganuzi wa Kimaeneo ya Fishman (1972). Data ya makala hii imechambuliwa kwa kutumia mkabala wa maelezo. Matokeo ya makala hii yamebainisha kuwa wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na kutumia msamiati sanifu pia hutumia misimu kutoka katika nyanja tofautitofauti katika mawasiliano yao ya kila siku. Mtafiti amechunguza misimu inayotokana na uwanja wa utani, soka na sanaa. Makala hii ni muhimu kwa wanaisimu kwani inabainisha misimu mbalimbali inayotumiwa na wanachuo wa chuo husika hususan kutoka nyanja za utani, soka na sanaa. Hii itatoa msukumo kwa wasanifishaji wa lugha ya Kiswahili kusanifisha misimu husika. Inapendekezwa kuwa watafiti wa lugha wachunguze misimuina yotumika   hivi sasa “2022-2023“, aina mbalimbali za misimu, misimu inayotumika katika maeneo mbalimbali kama vile shuleni, vijiweni, hospitalini, ofisini na kadhalika. Aidha, tafiti fuatizi zifanyike kuhusiana na vyanzo vingine vya misimu tofauti na vile vilivyoangaziwa katika makala hii, kwa mfano, ufanyike utafiti juu ya misimu itokanayo na michezo, siasa, milipuko ya magonjwa, matukio mbalimbali yanayojitokeza katika jamii, ndoa na kadhalika.


Journal Identifiers


eISSN: 2958-4914
 
empty cookie