Main Article Content

Mchango wa kasida teule za Zanzibar katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa virusi vya Korona


Ulfat Abdul-aziz Ibrahim

Abstract

Kasida kama aina mojawapo ya nyimbo zenye maudhui ya kidini zimekuwapo katika jamii zetu kwa muda mrefu. Kasida hizi hutumika katika matukio mbalimbali ya kijamii kama vile sherehe na misiba (Said, 2016). Kupitia kasida, jamii imekuwa ikielimika, kuburudika na kupata nasaha muhimu za maisha. Aidha, kwa kuwa kazi za sanaa, ikiwamo fasihi, ni zao la jamii, watunzi wa kasida za kidini pia husukumwa na matukio mbalimbali ya kijamii kutunga kazi zao. Kwa muktadha huo, makala hii inalenga kuchambua mchango wa kasida za dini katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Virusi vya Korona– 19 (kuanzia sasa UVIKO-19). Ili kusheheneza makala, mwandishi amesikiliza na kuchambua kasida teule zilizoimbwa kutoka vikundi na madrasa teule za Zanzibar. Ukusanyaji data na uchambuzi wake umeongozwa na Nadharia ya Uhalisia. Matokeo ya utafiti yameonesha kuwa kasida zina mchango mkubwa kwa jamii. Miongni mwa mchango huo ni pamoja na kukumbusha watu kumrejea Mungu, kutoa elimu ya kujikinga na UVIKO-19, kueleza hali ya upatikanaji wa huduma za afya, kubainisha athari za UVIKO-19 na kufanya maombi juu ya kutokomeza UVIKO-19. Kwa ujumla, makala imebainisha mchango wa kasida teule kwa jamii ya Wazanzibari, hususani katika kupambana na magonjwa ya mlipuko. Hivyo, mwandishi anapendekeza kuwa jamii iziendeleze kasida katika kutoa elimu ya kuikinga, kupunguza athari na kuifariji jamii dhidi ya
magonjwa mbalimbali ya mlipuko ukiwemo UVIKO-19.


Journal Identifiers


eISSN: 2591-7013
print ISSN: 2665-0789
 
empty cookie